Saturday, August 23, 2014

Tofauti kati ya Agano la Kale na Agano jipya







 Kuna tofauti kati  ya Agano la Kale na Agano jipya
·         Agano la Kale lilifanyika pasipo kiapo cha Mungu Baba [Waebrania 7:20]
·         Agano la Kale lilizuiliwa na mauti ya makuhani waliolifanya. Agano
Jipya Kuhani wake YESU KRISTO anaishi milele [Waebrania7:24]
·         Agano la kale lilifanyika kwa damu za wanyama ( kondoo, mbuzi na
ndama). Lakini Agano Jipya limefanyika kwa DAMU YA YESU [Mwanadamu Kristo Yesu] [ Waebrania 9: 12-21]
·         Agano la kale ni sheria inayotuonyesha Dhambi. Agano Jipyalinatoa suluhisho ya dhambi [ WOKOVU], Yohana 3:6
·         Agano la kale ni linatuonyesha HUKUMU ya dhambi, lakini Agano Jipya linatuonyesha NEEMA NA REHEMA ambayo iko juu ya sheria ya hukumu.
·         Agano la kale lina vitabu 39 na Agano Jipya lina vitabu 27

 Biblia ni kitabu cha Agano la Kwanza na la Pili chenye jumla ya maagano saba pamoja na agano jipya.
1.      Agano la Edeni [ Edenic Covenant]
2.      Agano la Adamu [ Adamic Covenant]
3.      Agano la Nuhu [ Noahamic Covenant]
4.      Agano la Musa [ Mosaic Covenant]
5.      Agano la Ibrahimu [Ibrahimic Covenant]
6.      Agano la Daudi [ Davidic Covenant
7.      Agano Jipya [New Covenant]
Agano lolote lina lina nguvu na kuna shehemu kuu tatu katika kila Agano kati
ya Mungu na Mwanadamu na kati Mwanadamu na Mwadamu. Mkataba
wowote unahusu sehemu kuu mbili za Mkataba. Sehemu kuu tatu za Agano ni
AHADI, MASHARTI NA MUHURI [PROMISE, CONDITIONS AND
SEAL] 
 
World Miracle Mission Center
 P .o Box 78620 Dar es salaa
 Tel 0754-69 20 19