UTANGULIZI:
I. Chanzo cha ndoa.
A. Mawazo mbali mbali kuhusu taasisi ya ndoa
ilivyoanza.
1. Hekaya ya
Kiafrika (Lesotho):
“Hapo kale walikuwepo vijana wanne ambao waliwinda pamoja daima. Hakuwepo mtu
mwingine duniani kwa jinsi hiyo waliwaza, lakini siku moja Mungu aliumba
mwanamke na akamfundisha kusema, kuoka mkate na kutengeneza vyungu, kuotesha
nafaka na kupika. Hatimaye siku njema moja ndugu hawa wanne wakakutana na huyu
msichana na walijiuliza, Je huyu ni
mnyama au binadamu. Mmoja wao akasema ninampenda na hivyo aliwazuia kaka zake
wasimtendee kama mnyama. Wale watatu waliondoka wakisema hitaji lao
lilikuwa ni kuwinda wanyama na kama ndugu yao
alimtaka mnyama yule (mwanamke)wao wangeendelea mbele kuwinda wengine kwa ajili
yao. Hawakuonekana
tena kwani baada ya miaka ya kuwinda walipokuwa wazee waliuwawa na simba
nyikani kwa kuwa hawakuweza kujihudumia na kujilinda. Kwa upande mwingine ndugu
yao aliyempenda
mwanamke aliishi na yule mwanamke ndani ya pango karibu na kisima miambani.
Mwanamke yule alimiliki moto hivyo alimpikia nyama, uji na mboga, ambavyo
alikuwa amevilima. Mwanamume alikuwa na furaha kuu na alilishwa vema mno.
Walipata watoto wengi na hata wajukuu, ambao waliwatunza katika uzee wao”
(Knappert 1990: 153)
2. Hekaya
ya Kihindi: Deerghatumma ambaye ni kipofu alisema ndoa yapaswa kumpa
mwanamume
mamlaka juu ya mwanamke.
a. Usemi huo ulitokana na ukweli
kuwa wanawake walikuwa na “mamlaka zaidi.”
b. Hata hivyo, endapo sababu ya
ndoa itakuwa ni kuruhusu wanaume watumie mamlaka vibaya, ndoa yapaswa kupigwa
marufuku kabisa.
3. Wengine
husema ya kuwa ndoa ilizuka tu kama vile mtu
alivyozuka:
a. Yasemekana ya kuwa ndoa ni
matokeo ya hitaji lihusianalo na utatuzi wa maswala ya malezi na matunzo ya
watoto.
b. Kwa hiyo endapo majukumu ya
ndoa yalizuka, yaweza kuendelea kuzuka na kubadilika na kuwa tofauti.
4. Endapo ndoa ni taasisi
iliyoanzishwa na wanadamu, na ikiwa imetokana na hekaya au kuchipuka kwa njia
ya asili tu, basi mwanadamu ana uwezo wa kubadili sheria zinazotawala ndoa au
hata kuachana nayo kabisa.
B. Neno
la Mungu laandika ya kuwa Mungu ndiye aliayenzisha ndoa (Mwz 2:18-25).
1. Yesu alinukuu kuhusu ndoa
iliyoanzishwa na Mungu katika Math 19:5.
2. Paulo alinukuu kuhusu ndoa
iliyoanzishwa na Mungu katika Efe 5:31.
3. Hivyo, hatuwezi kuibadili au
kuachana nayo. Wajibu wetu ni kutii asemacho Mungu kuhusiana na taasisi yake.
C. Kwa
njia ya ndoa Mungu hutimiliza kilicho chema kwa kumpatia mwanamume msaidizi wa
kumfaa.
1. “Si vema kwa mwanamume kuwa peke yake” (Mwz 2:18). Uumbaji wa
mwanadamu umefanyika katika hatua mbili (Mwanzo
2 hutoa maelezo ya kina ya uumbaji wa binadamu, ambao kwanza waelezwa
katika Mwz 1:26-27). Akiwa amesha
muumba mwanamume, ambaye kimaumbile aliandaliwa awe na mwenzi, yamaanisha:
a. Yalikuwapo
mambo zaidi ya kufanya—Kazi ya Mungu kuhusiana na mwanamume ilikuwa
haijakamilika: mwanamume aliumbwa na ameumbwa kuwa na mwenzi wa kuambatana
naye.
b. Mwanamume
mkamilifu paradiso (mahali pakamilifu) akiwa na chakula kizuri na kazi nzuri (Mwz 2:15), na Mungu mzuri, bado
hakuweza kujitosheleza yeye binafsi.
c. Binadamu aliumbwa kama kufuli na funguo—moja bila nyingine haina kazi.
d. Watu hutegemeana, sio
wakujitegemea (huru)
e. Kwa asili mwanamume na mwanamke
wanapaswa kuoana. Useja ni kipawa maalum kutoka kwa Mungu (1 Kor 7:7).
2. “Nitamfanyia msaidizi wakufanana naye” (Mwz 2:18). “Msaidizi wakufanana” yamaanisha “wa kukubaliana,” au “mwenzi” wa mwanamume,
kumkamilisha na kumsaidia, sio kuwa mtumwa wake. Hii inamaanisha:
a.Mwanamume anahitaji mwenzi wa
kuzungumza naye, kushiriki naye hisia, maono, furaha, huzuni, nk.
b. Uhitaji wa msaidizi kwa
mwanamume wadhihirisha kuwa mwanamume anahitaji msaidizi, wakumtegemeza, mshiriki,
rafiki.
c. Mwanamume anahitaji msaada ili
kuijaza nchi na katika jukumu la kuitiisha
nchi.
d. “Msaidizi”
ni cheo cha kuheshimika.
(1) Mungu mwenyewe wakati mwingine
huitwa “Msaidizi” (Zab 30:10; 40:17; Ebr
13:6).
(2) Yesu alimwita Roho Mtakatifu
“Msaidizi” wetu (Yoh 14:16, 26; 15:26; 16:7).
(3) Endapo cheo “Msaidizi” ni
chakumstahili muumba wa ulimwengu, basi hakiwezi kuwa na hadhi ya chini kwa mke.
Kinyume chake, ni cheo cha heshima, na
mke ajivunie kuwa nacho.
(4) Mume na mke wautazame Utatu
unao “saidiana” kuumba, kutawala, kufurahia, kuhuzunika, nk.
3. Mchakato aliotumia Mungu wa
kumpa Adam jukumu la kuwapa wanyama majina ulidhihirisha wazi kuwa hakuwepo
mnyama aliyefaa kuwa msaidizi wa mwanamume
(Mwz 2:19-20).
a. Bwana akamletea Adamu wanyama awape majina, yamaanisha,kutathmini sifa
na ubora wao. Adamu alitathmini sifa na ubora wao na kutokana na hizo
akawapa majina yaliyowastshili. Na mchakato huo ulidhihirisha kuwa “hakuwepo msaidizi wa kufanana naye” (Mwz 2:20).
b. Rabi Fulani anatupa picha hii—wanyama wanakuja kwa jozi: “Kila
mmoja ana mwenzi, ila mimi sina mwenzi.”
c. Huenda Adamu alishayagundua mahitaji yake ya ndani kutokana na jinsi
Mungu alivyomuumba—hitaji la mwenzi, usaidizi katika majukumu ya kimaisha,
hitaji la binafsi la kujamiiana. Hata hivyo, Adamu hakupata alichokihitaji
miongoni mwa wanyama kwani alichohitaji si mnyama.
d.
Matumizi: Wanaume, je mmeshatambua na kukubali kuwa hamjitoshelezi?
(1) Uliumbwa kwa namna ya kuwa
tegemezi kwa mkeo.
(2) Wapaswa pia kujua hitaji lako
la msaidizi haliwezi kutoshelezwa na chochote kile miongoni mwa vitu au wanyama.
D. Mungu
alimuumba msaidizi wa kumfaa mwanamume kutokana na mwili wa mwnamume (Mwz 2:21-22).
1. Mungu alimuumba msaidizi
wakati Adamu amelala. Kumbukumbu hazionyeshi kuwa Adamu alihusika kwa namna
yoyote katika mchakato wa uumbaji.
2. Adamu
hakujua namna ya kutatua hitaji lake la msaidizi.
3. Kutokana
na kusudi lake la milele na hekima yake Mungu alilitambua hitaji la Adamu hasa.
Ni yeye pekee ajuaye vigezo vilivyosababisha mwanamke awe msaidizi wa kufaa,
mwenzi, rafiki na mshiriki kwa mwanamume ili ile sura ya mfano wa Mungu
ionekane ndani yao.
4. Bwana huamua namna ya kukidhi
hitaji- nini kinafaa kuwa msaidizi wa mwanamume.
5. Mungu alimuumba msaidizi kwa
kutumia sehemu ya mwili wa Adamu, ubavu wake, mwili ambao ni tofauti na ule wa
wanyama. Inamaanisha:
a. Hapaswi kufananishwa na jamii
ya wanyama.
b. Yeye si hayawani mwenye
kutulemea, licha ya tamaduni nyingi kuwachukulia wanawake
kwa namna hiyo.
c. Hapaswi kupigwa, kwa viboko au
maneno.
6. Kama alivyosema mwenye hekima
mmoja, “Mwanamke hakutokana na sehemu ya kichwa cha mwanamume, asije
akamtawala, au hakutokana na sehemu ya miguu,asije kanyagwa naye, lakini katoka
ubavuni ili awe mshiriki kama mwenzi aliye
sawa naye ingawaje ana jukumu tofauti.”
7. Matumizi:
Mwenendo na tabia yako kwa mume au mke wako ikoje?
II. Asili na kusudi la ndoa.
A. Kwa asili, ndoa ni ya kiroho.
1. Ndoa
yawakilisha umoja kati ya washiriki watatu wa Utatu Mtakatifu (Baba, Mwana,
Roho Mtakatifu). Kama vile washiriki
watatu wa Utatu Mtakatifu walivyo nafsi tofauti bali Mungu mmoja, vivyo mume na
mke ni watu tofauti bali wameunganishwa na “kuwa mwili mmoja” (Mwz 2:24).
2. Ndoa ni
mfano wa uhusiano wa Yesu na kanisa lake (Efe
5:22-33).
a. Mke na amtii
mumewe kama kanisa linavyomtii Kristo.
b.
Mume na ampende mkewe kama Kristo
alivyolipenda kanisa akajitoa kwa ajili ya kanisa .
c. Kwa hiyo, wana ndoa wanapaswa
kuwa mfano ulio hai na wazi wa uhusiano wa Kristo na kanisa lake.
B. Ndoa ni taasisi ya msingi na
kiini cha jamii ya wanadamu.
Kuvunjika kwa ndoa (kupitia talaka,muunganiko
wa jinsia moja, na kujamiiana nje ya ndoa), ambavyo hutokana na kutofuata neno
la Mungu, huharibu utamaduni wa watu wa Magharibi na utafanya yayo hayo kwa
utamaduni wa watu wasio wa ki-Magharibi.
C. Kusudi la ndoa:
1. Kutokana na Mwanzo makusudi yafuatayo ya ndoa
hujitokeza:
a.
Urafiki (Mwz 2:18).
b.
Umoja (Mwz 2:24).
c.
Uzao (Mwz 1:28; 9:1, 7).
d.
Starehe (Mwz 3:16; tazama pia Mhu 9:9;
Wimbo ulio Bora 1-8; 1 Kor 7:3-5).
2. Pamoja na hayo Agano Jipya
laongezea makusudi yafuatayo ya ndoa:
a. Ulinzi dhidi ya uasherati (1 Kor 7:9).
b. Utakaso wa kibnafisi au
unaoendelea (Efe 5:26).
BY JONATHAN MENN
jonathanmenn@yahoo.com