.Waefeso 5.25….Enyi waume wapendeni wake zenu kama vile kristo naye alivyolipenda Kanisa…….!
Kati ya Mateso,uchungu na maumivu ambayo wanawake wengi hupitia ni ;
• Kujua Mawazo ya mwanaume kama kiongozi wa familia na maamuzi juu ya ndoa
• Kubeba ujauzito kwa miezi tisa nahata Zaidi
• Kuzaa kwa uchungu,Mateso na Maumivu makali,
• Kulea watoto Usiku na Mchana
• Kutunza usafi wa nyumba na Familia
• Kushiriki tendo la ndoa kwa Maumivu
Na ndiyo maana sisi wanaume tunaaswa kuwapenda wanawake na kuishi nao kwa akili 1Petro 3;7 Lakini yapo mambo ambayo husababisha Ndoa nyingi kuvunjika nayo ni:
• Mwanaume kutosimama kama kiongozi wa kiroho na kimaisha
• Mwanamke kukosa utulivu,utii na Upole .1 Petro 3;4-5
• Mwanaume kukosa sifa ya kuilinda na kutimiza mahitaji muhimu ya kimaisha(malazi,chakula na Malazi)
• Mwanaume kukosa sifa ya kutoa mwelekeo wa kiroho na kimaisha.
Roho Mtakatifu atupe Moyo wa toba na Kuliishi neno la Mungu katika Roho na Mwili,Usikate tamaa Mungu amesikia maombi yako na Yangu ila tufanye toba ili atusaidie.